John 12:3-8

3 aKisha Maria akachukua chupa ya painti moja
Painti moja ni kama nusu lita.
yenye manukato ya nardo
Nardo ni aina ya mafuta yaliyokuwa yanatengenezwa kutokana na mimea yenye mizizi inayotoa harufu nzuri.
safi ya thamani kubwa, akayamimina miguuni mwa Isa na kuifuta kwa nywele zake. Nyumba nzima ikajaa harufu nzuri ya manukato.

4 dNdipo Yuda Iskariote mwana wa Simoni, mmoja wa wale wanafunzi ambaye ndiye angemsaliti Isa, akasema, 5“Kwa nini manukato haya hayakuuzwa kwa dinari 300
Dinari 300 ni sawa na mshahara wa kibarua wa siku 300.
na fedha hizo wakapewa maskini?”
6 fYuda alisema hivi si kwa kuwa aliwajali maskini, bali kwa kuwa alikuwa mwizi, kwani ndiye alikuwa akitunza mfuko wa fedha akawa anaiba kile kilichowekwa humo.

7 gIsa akasema, “Mwacheni. Aliyanunua manukato hayo ili ayaweke kwa ajili ya siku ya maziko yangu. 8 hMaskini mtakuwa nao siku zote, lakini mimi hamtakuwa nami siku zote.”

Shauri La Kumuua Lazaro

Copyright information for SwhKC